Kanuni za Kuzingatia Katika Betting

Zingatia Kanuni hizi unapokuwa unapanga mkeka wako ili uweze kupata mafanikio mazuri katika soko hili mikeka.

Kanuni ya 1
Tafuta kampuni inayotoa huduma nzuri. Hii ni kanuni muhimu katika soko la mikeka. Ikiwezekana jiunge na makampuni mengi yanayoendesha ubashiri wa michezo mitandaoni (bookmakers/betting sites) kadiri uwezavyo ili mradi tu uwe umetimiza masharti yao. Hii itakusaidia kufanya chaguzi na kujua ni kampuni ipi inatoa huduma nzuri na odds nzuri zinazoweza kukupatia wewe faida kubwa. Kwa sababu wakati mwingine unakuta makampuni yanatofautiana katika upangaji wa odd zao. Using’ang’anie kampuni moja tu eti kwa sababu ndiyo umeizoea labda kama wanakupatia huduma nzuri inayokuridhisha.

Kanuni ya 2
Panga kiwango cha kuweka (mzigo). Baada ya kupata kampuni unayoona inafaa hatua inayofuata ni kujua kiwango gani unaweka kwa mkeka wako au utakachokuwa unatumia kuweka katika mikeka yako. Suala hili mara nyingi lina amuriwa na namna gani unajiamini katika kupanga mikeka yako (ubashiri wako) na faida unayoipata au tarajia kuipata. Kama hujawa mzoefu katika soko hili la mikeka usiweke kiwango kikubwa ambacho ikitokea umepoteza usiumie sana, labda uwe umeamua kujitoa muhanga (kujilipua) kwamba liwalo na liwe ama una uhakika/unajiamini na mkeka/mikeka yako.

Kanuni ya 3
Usiwe na papara au haraka.Unaweza ukawa umepigwa kwenye mikeka mingi na unataka kurudisha pesa yako kwa haraka unaona ligi kubwa zinachezwa leo ukakimbilia kuchagua timu kubwa kubwa na kuweka kiwango kikubwa ili faida yako irudi haraka; usijaribu kufanya hivyo. Tulia panga mkeka wako taratibu kwa umakini kama ulivyozoea, ikiwezekana acha kuweka mkeka kwa muda ujipange na kufikiria vizuri ndio urudi mchezoni. Ama wakati mwingine michezo inakaribia kuanza unakimbizana na muda kuweka timu unazoziaminia; usifanye hivyo pia.

Kanuni ya 4
Panga mkeka wa timu chache. Inatokea mara chache mtu kuweka timu nyingi kwenye mkeka mmoja na matokeo yote yakawa sahihi hata kama timu zote ni kubwa na unaziaminia huwa inatokea hata timu moja tu inakuangusha. Ingawa inashawishi kuweka timu nyingi kwenye mkeka mmoja kwani huwa inakuja faida kubwa lakini uhakika wa wewe kushinda pia unapungua tofauti na ukiwa umeweka timu chache, ingawa inatokea wakati mwingine hata kwa timu chache inatokea moja inakuangusha. Lakini ni bora badala ya kuweka timu nyingi kwa mkupuo kwenye mkeka mmoja unaweza kuzigawa hata kwenye makundi mawili au matatu ili kujiongezea nafasi ya kushinda.

Kanuni ya 5
Fuatialia habari za michezo unayopenda kuiwekea mikeka. Kama ni mpira wa miguu, kikapu, n.k. jaribu kuzifuatilia habari za michezo hiyo au hata kuwa unaangalia mara kwa mara kujua uwezo wa timu na aina ya ligi mbali mbali. Hii itakusaidia kujua kama wachezaji muhimu wa timu hawapo uenda wapo majeruhi au wapo nje kwa adhabu au wamehama, pia unaweza kujua historia za timu zinazokutana. Unaweza kukuta timu A inaongoza ligi na timu G inakaribia kushuka daraja lakini ukiangalia historia ya timu hizi mbili zikikutana huwa inakuwa ngumu kwa timu A kuifunga timu G kirahisi, kwa hiyo kama wewe ni mfuatiliaji itakusaidia kufanya maamuzi mazuri katika kupanga mkeka wako.

Kanuni ya 6
Chagua aina ya mkeka unaoweka kwa makini. Kuna wengine wanapenda kubet magoli, wengine matokeo ya kipindi cha kwanza tu, wengine matokeo ya vipindi vyote (HT/FT), wengine matokeo ya mchezo wote n.k. Kwa hiyo inakupasa kuchagua kwa makini aina mkeka unaotaka kuweka sio tu kuangalia sehemu utakayopata faida kubwa. Na hapa kufutilia michezo na kuzijua timu unazozibashiria kuna saidia sana, kwani unaweza kukuta timu A na G huwa hazifungani magoli mengi au lazima kila timu ipate goli zikikutana kwa hiyo ukaamua kubet magoli.

Kanuni ya 7
Kuwa na staha. Usiwe na tamaa ya kutaka kupata faida kubwa kwa mara moja ni hatari sana kwani inaweza kupelekea ukawa unapata hasara kila siku. Cheza kwa kiasi na wakati mwingine unapoona kwamba mambo hayaendi vizuri unaweza kupumzika kwa muda ujipange vizuri. Jaribu kucheza mikeka michache yenye uhakika hata kama unapata faida kidogo ni bora kuliko kwenda kwa pupa na kupoteza hata ulicho nacho. Ingawa kupoteza nae ni sehemu ya mchezo huu lakini siyo upoteze kizembe namna hiyo.

Kanuni ya 8
Tunza kumbukumu ya mikeka yako. Hii ni muhimu sana kwani itakuonyesha ni faida kiasi gani unapata au ni kiasi gani umepoteza. Itakusaidia kupanga hatua inayofuata, unaweza kuamua kuacha kwa muda kama unapata hasara au ukaamua kubadilisha mbinu za uchezaji.

Kanuni ya 9
Kuwa na msimamo na unachokijua. Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri na unaijua vizuri ligi ya Uingereza ni vizuri ukawa unapendelea kubashiri michezo ya ligi hiyo sana kuliko ligi nyingine ambazo huzijui vizuri. Sio kwa sababu katika kuperuzi peruzi ukaona kuna timu hapo katika ligi ya Scotland imepewa odd za kuvutia ukaamua kuiwekea mkeka, unaweza ukapotea.

Kanuni ya 10
Usidanganywe na matokeo ya muda mfupi. Kwa mfano Leicester City imeshinda michezo mitano mfululizo, jiulize “ni kwa sababu timu yao ni timu bora na nzuri au wamebahatisha tu?”. Kama unaamini timu yao ni bora na nzuri unaweza kuendelea kuwabashiria ushindi, lakini kama unaona na unaamini wanabahatisha tu tafakari kwa makini kabla hujaamua kuwatabiria ushindi. Hapa kuzijua ligi na timu vizuri pia huwa kuna saidia sana. Kuna baadhi ya timu huwa zinafanya vizuri wakati ligi zinaanza msimu wa kwanza lakini kufikia msimu wa pili hazifanyi vizuri, hii pia huchangiwa na kukuta baadhi ya wachezaji muhimu wamehama timu. Kwa hiyo ni vizuri kuwa mfuatiliaji.

Post a Comment

Previous Post Next Post