Mchezo wa kubashiri (Betting) ni mchezo ambao umeweza kujizolea umaarufu mkubwa hivi karibuni na sio ndani ya Tanzania pekee, bali kwa ulimwengu mzima kwa ujumla. Watu wengi wamekuwa wakiutumia mchezo huu kwa kujiingizia kipato kwa cha muda mfupi (short term) au cha muda mrefu (long term). Na kuna baadhi ya watu wamefikia hatua ya kufanya kama ndio ajira yao au sehemu yao kuu ya kuingizia kipato. Mbali ya watu kujifurahisha na kunufaika na michezo hii wengine kwao mchezo huu wa kubashiri umekuwa mwiba mkubwa na janga kwao kufuatia kuwapatia hasara kubwa baada ya kupoteza pesa nyingi bila ya kupata faida yoyote hivyo kuwaacha katika hali ngumu zaidi. Na watu wengi wamekuwa wakipata hasara kubwa katika mchezo huu kufuatia kutojua namna ya kucheza kwa kwa umakini na staha ili uweze kuwaletea faida badala ya hasara. Wakubet baada ya kufanya utafiti na kufanya uchambuzi kwa kina imegundua njia zifuatazo zikifuatwa kwa makini zinaweza kusaidia mchezaji kwa kiwango kikubwa kupata faida badala ya hasara. Njia hizo ni:
1. Usiufanye Mchezo huu kama chanzo chako kikuu cha mapato
Usiufanye mchezo huu wa kubet kama chanzo chako kikuu cha mapato cha kutegemea. hii itakuepusha wewe kutoshusha kipato chako hata endapo utapata matokeo ambayo hukuyatarajia katika mchezo huu,
2. Usitumie fedha zako Muhimu kubet
Kamwe usipende kutumia fedha zako muhimu kubet. Kwa mfano pesa za kuendeshea maisha na familia yako kila siku, pesa za ada za shule, pesa za kuhudumia mgonjwa n.k. Tumia pesa za ziada ambazo unazipata, pesa ambazo ungeweza kwenda kunywa bia na marafiki au pesa ambayo ungeweza kutumia hata kwenye starehe. Hii itakusaidia kuendelea na maisha yako kama kawaida hata endapo kama mambo yataenda tofauti kwenye betting.
3. Jaribu kuzifuatilia uzijue vyema timu unazobashiria
Ni vyema ukazifuatilia kwa makini timu zote ambazo unazibetia ili uweze kupunguza hatari ya kupoteza mara kwa mara na pia kukupa uwezo wa kufanya uchaguzi sahihi. Kwa mfano unaweza kujua kuwa Liverpool na Arsenal wanapokutana mara nyingi lazima wafungane hivyo badala ya kuweka fulani anashinda au wanatoka droo unaweza kuweka kuwa timu hizi lazima zifungane (GG/BTTS).
4. Weka timu chache unazoziamini
Unapoweka timu chache unazoziamini unapunguza uingiwezekano wa kupoteza. Japokuwa inawezekana usipate fedha nyingi lakini usalama wa pesa yako na uhakika wa ushindi unakuwa mkubwa zaidi.
5. Usibashiri kwa Mapenzi ama ushabiki
Usibashiri kwa mapenzi ama ushabiki, eti kwa kuwa mimi ni mshabiki wa Arsenal basi ndo nakuwa naitabiria ushindi kila mara, angalia uwezo wa timu yako dhidi ya timu pinzani kama inaweza shinda na hii itakuwa rahisi endapo utakuwa mfuatiliaji mzuri pia wa ligi ama mchezo unaobashiri.
6. Cheza kwa kiasi Mchezo huu
Usiwe na tamaa kwamba unaweza pata pesa nyingi kwa mara moja kwahiyo ukacheza hovyo bila mpangilio, hutaumia. Jaribu kuweka mikakati na mipangilio juu ya uchezaji wako, hakika hutajuta. Cheza mechi chache kwa siku unazoamini zinaweza kukupatia ushindi sio lazima ubashiri mechi nyingi kwa mkupuo. Hii itakusaidia wewe kukupa ushindi mara nyingi.
7. Jifunze zaidi
Siku hizi kuna vyanzo mbalimbali vya kuweza kujifunza kama vile mtandao, mitandao ya kijamii, vitabu na hata kupitia watu. Hivyo ni vyema pia mtu ukawa unajifunza zaidi kuhusiana na mambo haya ya kubet ili uweze kupunguza kupata hasara na kupata faida zaidi.